Viongozi wa kiarabu kuijenga Gaza mpya

CAIRO: VIONGOZI wa Kiarabu wamepitisha mpango wa Misri wa kuijenga upya Gaza, utakaogharimu dola bilioni 53. Mpango huo utazuia kuwahamisha Wapalestina kutoka eneo hilo.
Pendekezo hili linatofautiana na maono ya Rais wa Marekani, Donald Trump, ya kutengeneza kile alichokiita eneo la mapumziko la Mashariki ya Kati.
Rais wa Misri, Abdel Fattah al-Sissi, amesema pendekezo hili, ambalo limekaribishwa na Hamas na kukosolewa na Israel, limekubaliwa wakati wa kuufunga mkutano wa kilele wa Cairo Jumanne. Alisema Misri imeshirikiana na Wapalestina katika kuunda kamati ya utawala ya wataalamu wa Kipalestina walio huru, watakaokabidhiwa utawala wa Gaza baada ya kumalizika kwa vita.
Rais wa Mamlaka ya Palestina, Mahmoud Abbas, amelikaribisha pendekezo hili la Misri na kumuomba Rais wa Marekani, Donald Trump, kuunga mkono mpango huu ambao hautahusisha kuwahamisha wakaazi wa Kipalestina. SOMA: Misri , Jordan kushirikiana kuijenga GAZA



