Israel yasitisha huduma ya umeme Gaza

ISRAEL : SERIKALI ya Israel imesitisha usambazaji wa umeme katika Ukanda wa Gaza huku ikijaribu kuishinikiza Hamas kukubali kuongezwa muda wa awamu ya kwanza ya makubaliano ya kusitisha mapigano.

Makubaliano ya kusitisha mapigano kati ya Israel na Hamas kimsingi yalimalizika mwishoni mwa wiki iliyopita. SOMA: Misri , Jordan kushirikiana kuijenga GAZA

Eneo hilo limeharibiwa kwa kiasi kikubwa na kampeni ya kijeshi ya Israeli tangu shambulizi la Oktoba 2023 na baadhi ya wasambazaji wamekuwa wakisambaza umeme kwa kutumia majenereta na nguvu ya jua.

Wakati huohuo, Kundi la Hamas limeitisha makubaliano ya awamu ya pili ya kusitisha mapigano, ambayo yanalenga kupata suluhisho la kudumu la mapigano.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button