Biteko awasili Barbados kunadi nishati safi kimataifa

NAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk Doto Biteko amewasili Barbados kushiriki Mkutano wa Kimataifa kuhusu matumizi ya nishati endelevu utakaofanyika katika mji mkuu wa nchi hiyo, Bridgetown kuanzia Machi 12 hadi 14.

Katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Grantley Adams nchini humo, Dk Biteko amepokelewa na Waziri wa Nishati wa Nchi hiyo, Lisa Cummins pamoja na Balozi wa Tanzania, Cuba na mwakilishi katika eneo la Caribean, Humphrey Polepole.

Aidha, Dk Biteko atashiriki katika majadiliano mbalimbali kuhusu matumizi ya nishati endelevu kimataifa ikiwemo nishati safi ya kupikia ambayo ni ajenda muhimu kwa ajili ya kuwakomboa wananchi dhidi ya matumizi ya nishati isiyokuwa safi.

Dk Biteko ameongozana na Mshauri wa Rais masuala ya Wanawake-Angellah Kairuki, Waziri wa Maji, Nishati na Madini Zanzibar-Shaib Hassan Kaduara na Katibu Mkuu Wizara ya Nishati-Felichesmi Mramba.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button