Japan yakwamisha ndoto za Tanzania futsal

UFILIPINO; TIMU ya taifa ya wanawake ya mchezo wa Futsal ya Tanzania, imeaga michuano ya kombe la dunia baada ya kufungwa mabao 9-0 na Japan kwenye Uwanja wa Philsports mjini Manila, leo Novemba 29, 2025.
Michuano hiyo inafanyika kwa mara ya kwanza na Tanzania ikiwa miongoni mwa timu zilizoweka historia kushiriki baada ya kukata tiketi yake ya ushiriki kwenye michuano ya Afrika nchini Morocco Mei mwaka huu.
Mechi ya leo ilikuwa ya kumaliza Kundi C na Tanzania ilihitaji ushindi kusonga mbele kwenye michuano hiyo.
Kwa ushindi huo Japan inaungana na Ureno kufuzu robo fainali kutoka Kundi C, huku Tanzania ikimaliza ya tatu kwa pointi zake tatu na New Zealand ikimaliza bila pointi baada ya kufungwa mabao 10-0 na Ureno katika mechi yake ya mwisho leo.
Katika mechi hiyo, Tanzania ilianza vizuri lakini kasi na maarifa ya wachezaji wa Japan vilifanya timu hiyo kwenda mapumziko wakiwa mbele kwa mabao 3-0 kabla ya kumalizia mabao sita kipindi cha pili.
Akizungumza baada ya mechi hiyo Kocha Mkuu wa timu ya Tanzania Curtis Reid alisema anafurahi kuona wachezaji wake wameimarika zaidi na wanatakiwa kujivunia kwa hilo.

“Sio kila mtu anaweza kucheza kombe la dunia, lakini wao (wachezaji) wameweza… ninachofurahi zaidi ni kwamba wanaimarika, hata kama tunapoteza mechi lakini naona mabadiliko kwao,”alisema.
Alilishukuru Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kwa kutoa sapoti kubwa kwa timu hiyo na kuiomba iendelee kuweka mikakati ili mchezo huo uchezwe.
Mechi za robo fainali zinatarajiwa kuanza kuchezwa Desemba mosi kwa Argentina kumenyana na Colombia, Hispania na Morocco na Brazil dhidi ya Japan.
Timu nyingine zitakazokutana kwenye hatua hiyo zinatarajiwa kujulikana baadae leo baada ya kumalizika kwa mechi za hatua ya makundi.




I make up to $90 an hour working from my home. My story is that I quit working at Walmart to work online and with a little effort I easily bring in around $40h to $86h… Someone was good to me by sharing this link with me, so now i am hoping i could help someone else out there by sharing this link…
.
More Details For Us→→→→→→→→→ http://Www.Cash43.Com
Google is now paying $300 to $500 per hour for doing work online work from home. Last paycheck of me said that $20537 from this easy and simple job. Its amazing and earns are awesome. No boss, full time freedom and earnings are in front of you. This job is just awesome. Every person can makes income online with google easily……….
.
More Details For Us→→→→→→→→→→ http://Www.Payathome9.Com