Mchuano mkali kukwepa kushuka daraja Ligi Kuu Bara 2024/25

LIGI Kuu Tanzania Bara imefikia hatua ya mzunguko wa pili, ambao ni wa kufa au kupona, huku kukiwa na idadi  kubwa ya timu zikipambana kuwania kutoshuka daraja.

Timu ya KenGold ya Chunya, Mbeya, iliyopanda daraja iko mkiani kwa muda mrefu, hivyo inapambana kujinasua kutoka katika nafasi hiyo ya hatari.

Timu hiyo, ambayo inashiriki ligi hiyo kwa mara ya kwanza, ilifanya mageuzi makubwa katika dirisha dogo la usajili kwa kusajili wachezaji wengi kuliko timu yoyote inayoshiriki ligi hiyo yenye timu 16.

Sehemu ya wachezaji wa Kagera Sugar

KenGold baada ya kusajili dirisha dogo, angalau imebadilika imefikisha pointi 16 baada ya kucheza mechi 23 kama timu zingine nyingi na kutoa tishio kwa timu zingine zinazoshiriki ligi hiyo pendwa hapa nchini.

Ukiondoa Yanga, Simba, Azam na Singida Black Stars iliyopo nafasi ya nne.

Kimahesabu, KenGold inahitaji miujiza ili kujiepusha na janga la kushuka daraja, lakini watu wasiichukulie poa kwani ikipambana vizuri, inaweza kufikisha pointi 37 kama ikishinda mechi zake zilizobaki na kuifikia Tabora United ya Tabora iliyopo katika nafasi ya tano, kama ikifungwa mechi zake zote saba zilizobaki.

Matokeo hayo yamesababisha au kuzua hofu sio tu kwa timu zinazosubiri kucheza nayo, ila pia na kwa timu 11.
timu hizo zilizomo katika hatari ya kupitwa na KenGold kama zitachanga karata zake vibaya ni pamoja na Tanzania Prisons ya Mbeya,

Kagera Sugar ya Kagera, Pamba Jiji ya jijini Mwanza, Namungo ya Lindi na KMC ya Dar es Salaam. Timu zingine  zilizopo katika hatari hiyo ni Mashujaa ya Kigoma, Coastal Union au ‘Wana Mangushi’ ya jijini Tanga, Dodoma Jiji ya Dodoma, Fountain Gate ya Manyara, JKT ya Dar es Salaam na Tabora United ya Tabora.

Kikosi cha Pamba Jiji

Timu hizo zisijisahau, kwani lolote linaweza kutokea na kuifanya KenGold kung’ara na baadhi ya timu kuishia hatua ya kucheza hatua ya mtoano au zingine zikashuka daraja kutegemeana na matokeo yao

Mpambano wa ubingwa

Kuna mpambano mkali wa kuwania ubingwa kwani Yanga, ambayo ndio bingwa mtetezi wa taji hilo, inapambana vikali kuhakikisha inachukua tena taji hilo huku Simba ikifukuzia kwa karibu kutaka kupoka taji hilo, ambalo inalisaka kwa muda mrefu.

Timu zingine zinazowania taji hilo, ambazo kwa sasa kama zitaendelea na kasi yake ni pamoja na Azam FC, Singida Black Stars na Tabora United, kwani zikigangamala zinaweza kupata moja kati ya nafasi nne za kwanza na kuambulia
moja ya nafasi za kushiriki mashindano ya CAF.

Lakini katika ubingwa, bingwa mtetezi Yanga ndio anapewa nafasi kubwa ya kutetea taji lake kwa mara ya tano mfululizo kutokana na makali yake ya kutoa kichapo cha maana kwa baadhi ya timu na hivyo hadi sasa kuwa na mabao 58 na pointi 58.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button