Shirika laandaa semina usalama wa chakula

SHIRIKA la Agrithaman kwa kushirikiana na Shirika la Kimataifa Global Alliance for Improved Nutrition (GAIN) linalojihusisha na maswala ya lishe wameandaa semina kuhusu salama wa chakula ili kujenga uelewa kwa jamii kuhusu usalama wa chakula.

Jumla ya washiriki 180 Bukoba Mjini wamehudhuria ambao ni viongozi wa soko kutoka kata  za Kashai, Rwamishenye, Bakoba Custom, Nyakanyasi na Soko Kuu, wawakilishi wa wauza nbogamboga, matunda na samaki.

Viongozi wa serikali kutoka kwenye mitaa na kata zenye masoko, viongozi wanawake 2 wa mitaa yote maafisa kutoka manispaa wa idara za afya  lishe, kilimo, na mifugo ili kupata uelewawa pamoja kuhusu maswala ya usalama wa chakula.

Mkurugenzi wa Shirika la Agrithaman Mbunge wa Viti Maalum Chama Cha Mapinduzi (CCM) anayetokana na NG,o Neema Rugangira akifungua mafunzo juu ya maswala ya usalama wa Chakula aliwaambia washiriki kuwa mafunzo hayo yametokana na kufanya ziara katika maSoko na Kuona namna ambavyo wauzaji wa mboga mboga na vyakula vya nafaka wanavyohifadhi vyakula isivyo salama hivyo shirika likawashirikisha wadau ambao wanaweza kutoa elimu bora juu ya kuhifadhi vyakula na mboga mboga.

“Tumekuwa tukila chakula Kila siku na matunda lakini kama hatuwezi kuhifadhi vizuri chakula ni kazi bure lengo la mafunzo haya ni kuandaa mabalozi bora ambao wanaweza kutumika kuwafundisha wananchi wote namna nzuri ya kuhifadhi chakula na kujua ni kwa jinsi gani wananchi wanaweza kitambua chakula na matunda yaliyoribika ili yasitumike na kuondoka changamotoo za kiafya hasa kansa na vifo  ndio maana tumechukua viongozi katika masoko yote ya Bukoba na viongozi wa kata zote 14” amesema Lugangira.

Aliwaambia washiriki wote kuwa Kwa kuwa bado ni kiongozi wa Bukoba kupitia uongozi na wadau mbalimbali anafanya jitihada kama kiongozi kuhakikisha Bukoba Mjini inakuwa mfano wa kuingwa katika usalama wa chakula  kwenye masoko yao

Reticia Ishengoma ofisa wa maswala ya sera na chakula kutoka Shirika la  Kimataifa la GAIN amesema kuwa shirika hilo lilishafaya utafiti na kugundua kuwa wananchi wengi wa Tanzania wanaopata magonjwa ya Kansa yanayotoka na uhifadhi mbaya wa vyakula wanatokea Kanda ya Ziwa ikiwemo mkoa wa Kagera hivyo wananchi wanapaswa kuwa makini  kwa njia wanazotumia kuhifadhi chakula.

Alisema katika masoko matano ambayo ameyapitia Bukoba mjini alikuta baadhi ya wauza matunda na mboga mboga wakitumia dawa katika bidhaa na bidhaa hizo zikiendelea kuuzwa sokoni huku akisema  kuwa vyakula vingi vya Nafaka kama mahindi na Karanga vinavyouzwa sokono  vikohatarini kupata  Sumu kuvu kwa asilimia kubwa kwani njia inayohifadhi bidhaa hizo sio salama

Katibu tawala wa Wilaya ya Bukoba Proscovia Mwambie amesema kuwa kupitia ofisi ya mkuu wa wilaya kwa kusaidia na viongozi walipata mafunzo haya wataweka utamaduni wa kutembelea  masoko na kutoa elimu kwa wananchi juu ya kutambua vyakula vilivyoharibika  na jinsi ya kuhifadhi vyakula kwa usalama ili kujenga kizazi bora

Mafunzo hayo yalitoa fursa kwa washiriki kueleza changamoto za kuhifadhi vyakula na namna bora lakini pia washiriki walifundishwa madhara makubwa yatokanayo na  matumizi ya vyakula ambavyo  havijahifadhiwa vizuri na jinsi ya kuepuka ikiwemo kuboresha lishe za watoto wao kupitia vyakula vyao.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button