Rais Kagame ailaumu Ubelgiji kuchonganisha Afrika

RWANDA : RAIS wa Rwanda, Paul Kagame, ameilaumu Ubelgiji kwa kuchonganisha Rwanda na mataifa mengine ya Afrika, na kusema yuko tayari kukabiliana na nchi hiyo ya Ulaya.

Akizungumza mjini Kigali, Rais Kagame alisisitiza kuwa Ubelgiji, ambayo ilikuwa mkoloni wa Rwanda na DR Congo, imekuwa mstari wa mbele katika kuhamasisha vikwazo dhidi ya Rwanda.

“Ubelgiji imeua raia wa Rwanda kwa miaka mingi. Wameendelea kufanya hivyo kila wakati wanarudi na kuondoka, tumeendelea kuwaonya kwa miaka mingi, na sasa tunawajulisha tena,” alisema Kagame.

Vikwazo dhidi ya Rwanda vimeendelea kuongezeka kutoka kwa mataifa makubwa duniani, wakilenga tuhuma za Rwanda kusaidia kundi la waasi la M23 linalopigana Mashariki mwa DR Congo.

Rais Kagame aliwahakikishia wananchi wa Rwanda kuwa nchi hiyo iko tayari kukabiliana na vikwazo hivyo. SOMA: Ujerumani kusitisha misaada Rwanda

Mzozo wa Rwanda na Ubelgiji umekuwepo kwa muda mrefu, na bado ni changamoto kwa diplomasia za mataifa ya Afrika.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button