Ujerumani kusitisha misaada Rwanda

UJERUMANI : SERIKALI ya Ujerumani imesema imepanga kusitisha misaada mipya kwa Rwanda kutokana na mashambulizi ya kundi la M23 mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.
Watalaamu wa Umoja wa Mataifa wanasema waasi hao wanasaidiwa na wanajeshi wa Rwanda. Taarifa kutoka wizara ya maendeleo ya Ujerumani itazuia ushirikiano na Rwanda.
Mbali na kusitisha msaada mpya wa kifedha, wizara hiyo imesema itatathmini ushirikiano uliopo kwa sasa wa maendeleo na serikali ya Rwanda. Msaada wa wizara ya maendeleo ya Ujerumani kwa Rwanda ni wastani wa euro milioni 50 kwa mwaka.
Wakatihuohuo, Wizara ya mambo ya nje nchini Rwanda imesema kuwa uamuzi wa Ujerumani kuingiza siasa katika ushirikiano si jambo lenye tija . SOMA: Canada yaiwekea vikwazo Rwanda
Hatua ya Ujerumani imejiri baada ya Uingereza hivi karibuni kusitisha msaada wake wa moja kwa moja kwa Rwanda na Canada ikaiwekea vikwazo nchi hiyo kuhusiana na mzozo huo.



