Dk. Mwinyi akabidhi sadaka Pemba

PEMBA : RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi amewashukuru na kuwapomgeza wadau mbalimbali waliojitokeza kujitolea sadaka kwa watu wenye mahitaji Maalum katika kipindi hiki cha Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.
Rais Dk.Mwinyi amesema hayo alipokabidhi sadaka mbalimbali zilizotolewa na Mfanyabiashara Said Nassir Nassor(Bopar) kwa wananchi wa Chanjamjawiri Wilaya ya Chakechake, Mkoa wa Kusini Pemba tarehe 19 Machi 2025.




