Mali yajiondoa mataifa ya Francophonie

BAMAKO: SERIKALI ya Mali imetangaza rasmi kujiondoa katika Muungano wa Kimataifa wa Nchi Zinazozungumza Kifaransa (Francophonie), hatua inayofuata baada ya majirani zake, Niger na Burkina Faso, kuchukua hatua kama hiyo.

Katika barua aliyoandika Waziri wa Mambo ya Nje wa Mali kwa mwenzake wa Ufaransa, Mali imetuhumu Ufaransa kwa kuiwekea vikwazo na kudharau uhuru wa nchi hiyo. Taarifa hiyo ilitolewa jana na shirika la habari la AP.

Hatua ya Mali inaendelea na ile ya Burkina Faso na Niger, ambazo pia zilijiondoa katika muungano huo siku chache zilizopita. Nchi hizi tatu zimekuwa na mgogoro mkubwa na Ufaransa baada ya mapinduzi ya kijeshi, ambayo yamevuruga uhusiano wa kidiplomasia na kusababisha nchi hizo kufukuza wanajeshi wa Ufaransa.

Francophonie tayari imezisimamisha nchi hizi tatu kutokana na mapinduzi ya kijeshi. Uamuzi huu unaonyesha mabadiliko makubwa katika ushirikiano wa kisiasa na kijeshi, huku Mali na majirani zake wakielekea zaidi kwenye ushirikiano na Urusi badala ya Ufaransa.

SOMA: Ecowas yaitaka Senegal kupanga upya tarehe ya uchaguzi

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button