Rais Tinubu atangaza hali ya hatari Rivers

NIGERIA: RAIS wa Nigeria, Bola Ahmed Tinubu, ametangaza hali ya hatari katika jimbo la Rivers kufuatia mapigano ya kisiasa yaliyozua mgogoro mkubwa na kuvunja bunge la jimbo hilo.
Mvutano ulianzia Desemba 2023, baada ya viongozi 27 wa eneo hilo, watiifu kwa gavana wa zamani, kuhamia chama tawala cha APC. Hali hiyo ilisababisha gavana wa Jimbo la Rivers, Siminalayi Fubara, kulivunja bunge la jimbo tarehe 13 Desemba.
Rais Tinubu amechukua hatua hiyo baada ya kuona kuendelea kwa mzozo kati ya gavana mpya, Fubara, na mtangulizi wake, Ezenwo Nyesom Wike, ambaye sasa ni waziri.
Rais amemteua Ibokette Ibas kuwa mkuu wa serikali ya muda kwa miezi sita, huku gavana Fubara, naibu wake Ngozi Odu, na wabunge wateule wakisimamishwa kazi.
SOMA: NIGERIA: Hatma ya Burkina Faso, Mali na Niger kujulikana kesho



