Mradi wa SGR Isaka – Mwanza wabadilisha maisha ya wananchi

WANANCHI zaidi ya 13,000 kupitia Mradi wa Kimakakati wa Ujenzi wa Reli ya Kisasa ( SGR) kituo cha Mwanza mpaka Isaka (LOT 5 ) wameweza kunufaika kwa kujenga nyumba za kisasa na kumudu kununua mahitaji kwenye familia zao.

Meneja wa mradi kupitia kituo hicho, Mhandisi Christopher Kalisti amesema hayo alipozungumza na waandishi wa habari kwenye eneo la mradi  kata ya Sekebugoro Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga.

Mhandisi Kalisti amesema licha ya manufaa hayo wameweza kuongeza thamani ya ardhi zao zikiwemo halmashauri kuwa na mikakati ya mipango na kutangaza uuzwaji wa viwanja huku mzunguko wa fedha ukionekana kwenye maeneo hayo.

“Kwa kuanzia Isaka hadi Mwanza kutakuwa na vituo vya stesheni kumi vipo vidogo vidogo na vikubwa mojawapo Stesheni ya Malampaka inyochojumuisha mikoa ya Simiyu,Singida na Mara na kituo cha Fela kilichopo Mwanza ambapo kitatumika kuunganishia na kupaki mizig,”amesema Mhandisi Kalisti.

Mhandisi Kalisti amesema mpaka sasa ujenzi wa kunyanyua reli, kuweka mataluma, kupanda nyasi kando kando ili kuzuia mmommonyoko wa udongo kazi zote zimefikia asilimia 63 huku wakiweka alama za vivuko vya mifugo maeneo yenye mifugo mingi.

Mhandisi Kalisti amesema katika utekelezaji wa ujenzi huo wameweza kutoa elimu ya kuwaeleza manufaa ya mradi na kuwahimiza wa pande miti ili kuilinda miudnombinu.

Diwani wa kata ya Sekebugoro Fredinandi Mpogomi amesema Mradi huo umeweza kuwaleta wakandarasi ambao wameweka mikakati ya kutoa huduma kwenye jamii (CSR) kwa Sh milioni 165 kwa ajili ya ujenzi wa zahanati kwenye kijiji cha Sekeididi.

“Kijiji hiki hakina maji wakandarasi wanaotekeleza mradi huo walichimba visima kumi ambavyo waliomba visima vitatu waachiwe ili kuweza kuwanufaisha wananchi kupata huduma ya maji safi sababu hakuna chanzo kingine cha maji,” amesema Mpogomi.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button