Mpanzu: Simba tulieni

KIUNGO mshambuliaji wa Simba, Elie Mpanzu amesema anaamini bado hajaonesha uwezo wake wote katika timu hiyo.
Mpanzu ambaye ni raia wa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC), alijiunga na Wekundu wa Msimba dirisha dogo la usajili akiwa mchezaji huru baada ya kumaliza mkataba wake na As Vita, inayoshiriki Ligi Kuu ya nchi hiyo.
Mpaka sasa ameshaichezea Simba kwenye mechi za Ligi Kuu na Kombe la Shirikisho la CRDB, huku akifanikiwa kufunga mabao matatu Ligi Kuu.
Akizungumza hivi karibu jijini Dar es Salaam, Mpanzu alisema bado hajatoa 100% ya uwezo wake ingawa amejiunga na timu hiyo katikati ya msimu.
“Nimeanza ligi katika ya msimu, siwezi kuzungumzia sana kiwango changu ila bado sijatoa hata 80% ya uwezo wangu kuisaidia timu yangu, lazima inichukue muda kidogo ili niweze kuzoea ligi na mazingira yake kwa ujumla,” alisema Mpanzu.
Simba inajiandaa na mchezo wa robo faibali Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Al Masry ya Misri, Aprili 2, 2025.




nahitaji historia za wachezaji