CAG: Kuna maofisa wamekaimu miaka mitano

DODOMA — Ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kwa mwaka wa fedha 2023/24 imeibua hoja nzito kuhusu usimamizi wa rasilimali watu katika mashirika ya umma.

Takwimu zinaonesha kuwa watumishi 135 katika mashirika 19 ya umma wamekuwa wakikaimu nafasi kwa muda wa zaidi ya miezi sita—wengine hadi miaka mitano! Hii ni kinyume na Kanuni za Kudumu za Utumishi wa Umma zinazotaka kaimu asizidi miezi sita.

Katika taasisi kama Bohari Kuu ya Dawa, Chuo Kikuu cha Dodoma, Hospitali ya Taifa Muhimbili, na Mamlaka za Maji, hali hii inaathiri si tu morali ya wafanyakazi bali pia ufanisi wa huduma kwa wananchi. Watumishi wanaokaimu mara nyingi hukosa mamlaka kamili ya kufanya maamuzi, na hivyo kusababisha ucheleweshaji wa shughuli muhimu.

CAG anabainisha kuwa kuchelewa kwa mchakato wa uhakiki kutoka Ofisi ya Rais – Utumishi na Utawala Bora kunachangia hali hii, lakini pia kuna dalili za mashirika kutochukua hatua kwa wakati, ama kwa uzembe au sababu nyingine za kisiasa au kiutendaji.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button