Lundenga afariki dunia, Miss Tanzania wamlilia

MRATIBU wa zamani wa mashindano ya Miss Tanzania, Hashim Lundenga amefariki dunia leo Jumamosi April 19, 2025, huku waandaaji wa shindano hilo wakisema kifo chake ni pigo kwa fani ya urembo nchini.

Msemaji wa Miss Tanzania, Hiddan Rico amesema Lundenga atakumbukwa kwa mchango wake mkubwa kwenye tasnia ya urembo nchini.

“Taratibu za mazishi zinaendelea, lakini kwa taarifa nilizopokea huenda akazikwa kesho, ila muda si mrefu tutatoa taarifa kamili kuhusu mazishi yake, ”amesema na kuongeza kuwa msiba upo nyumbani kwa marehemu Bunju, Dar es Salaam.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button