Makini kushiriki uchaguzi mkuu 2025

CHAMA cha Makini kimesema kitashiriki Uchanguzi Mkuu Oktoba mwaka huu ili kulinda haki kila mtu kikatiba kwa kuchagua viongozi wanaowataka.
Kauli hiyo imetolewa leo Aprili 19, 2025 na Katibu Mwenezi Taifa wa Chama hicho, Fahmi Khalfan Abdalla wakati akitoa msimamo wa chama kuelekea uchaguzi huo wa Rais, wabunge pamoja na madiwani.
“Niseme wazi kuwa msimamo wa chama chetu nikushiriki kikamilifu katika uchaguzi mkuu utakaofanyika mapema mwezi oktoba mwaka huu na sababu kuu ni kulinda haki ya kila mwananchi kikatiba ambayo ni kupiga kura na kuchagua kiongozi anayemtaka kwani uchaguzi ni kwa ajili ya maslahi ya taifa hivyo tunashiriki ilitusiweze kupora haki hiyo,” amesema Abdalla.

Ameongeza: uchaguzi huu unatumia kodi za wananchi hivyo ilikuzilinda na kuzitumia vizuri ni lazima tushiriki uchaguzi kama haki ya msingi ya matumizi ya kodi zetu natoa wito kwa wananchama pamoja na wananchi kwa ujumla kuhakikisha wanajitokeza na kushiriki kikamilifu katika uchaguzi huo,”
Abdalla amesema chama kimekubaliana na kufikia uamzi kuwa wanawake waliotia nia pamoja na makundi maalum na watu wenye ulemavu kuchukua fomu za kumbea nafasi mbalimbali katika chama hicho bila malipo yoyote.
“Tunatambua mchango wa makundi haya ndani ya chama hivyo tumekubaliana hakuna gharama zozote zitakazotozwa kwa makundi haya zaidi fomu zitatolewa bure natoa wito kwao kujitokeza hata kama si mwanachama wetu lakini unawiwa na unania ya kuwania uongozi njoo ujiunge na fomu utapewa sharti uwe na vigezo kisheria,” amesema Abdalla
Aidha,Abdallah amevitaka vyama vya siasa na viongozi wake nchini kutunza amani ya nchi kwa kuepuka kutoa lugha za uchochezi kwani zinaweza kuchochea fujo na kuvuja tunu ya nchi (amani)hivyo kila kiongozi atimize wajibu wake.
Ameeleza kuwa ni wakati wa jamii kutopokea maneno na maelekezo ya nayoashiria uvunjivu wa amani,ili siasa na maendeleo yawezekufanyika ni laziama kuwe na amani na pia kunamaisha baada ya uchaguzi hivyo amani ilindwe kwa hali na mali.
Amesema mkutano mkuu wa chama hicho utafanyika mei 17, mwaka huu kwa lengo la kupitisha na kuitangaza rasmi ilani ya chama hicho na ndio utakuwa mwongozo wa uchaguzi pamoja na kupitisha wagombea wa urais Tanzania bara na visiwani na tayari watia nia wawili kutoka bara na mmoja zanzibar wamekwisha tia nia ya kugombea nafasi hiyo.
Katibu Mkuu Taifa wa Chama hicho, Ameir Hassan Ameir,amesema wamesaini maadili ambayo yatasaidia vyama vya siasa vitayasimamia katika uchaguzi huo hivyo wanachama wajitokeze kushiriki uchaguzi bila kuvunja sheria bali wakanadi sera za chama ilikuwashawishi wanachi kuwachagua na kuleta mabadiliko baada ya kuapishwa.

