CCM: Msikubali kununuliwa

ARUSHA: CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) kimewataka wanachama wake kutolukubali kununuliwa au kutumiwa na watu kwa maslahi yao binafsi, kikisitiza kuwa kitendo cha kununuliwa ni kudharauliwa.

Katibu wa NEC, Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa CCM Taifa, Kenani Kihongosi, ameeleza hayo leo Juni 5,2026 alipombele Shina Namba Nane katika Kata ya Lovilukuni wilayani Arumeru mkoani Arusha kukagua uhai wa chama.

Akizungumza na wanachama hao Kihongosi amewataka kutokubali kununuliwa au kutumiwa na watu wenye maslahi binafsi, akisema kitendo cha mwanachama kukubali kununuliwa ni ishara kwamba amedharauliwa na kupuuzwa utu wake.

“Niliwaambia hata watu wa Simanjiro msikubali kunuliwa kwa sababu ukiona unaweza kununua , ujue amekudharau, ukiona unaweza kuwekwa mfukoni na mtu, amekudharau na kiona mtu anakwambia maneno ya chuki ili umchukie mwenzako na unakubali, ujue amekudharau,” amesema.

Kihongosi amesema viongozi na wanachama wanapaswa kujenga utamaduni wa kuheshimu maamuzi ya chama, kulinda mshikamano na kuacha tabia zinazoweza kusababisha migawanyiko ndani ya chama.

Ameonya kuwa makundi ndani ya chama ni miongoni mwa mambo yanayoweza kudhoofisha nguvu ya CCM na kuathiri uwezo wake wa kutekeleza majukumu ya kuwatumikia wananchi.

“Tuepuke makundi ndani ya chama. Makundi yanaua chama, Lazima tuungane kukilinda, kukipenda na kukiheshimu Chama Cha Mapinduzi,” amesema Kihongosi.

Kihongosi amesisitiza kuwa nafasi na dhamana walizonazo viongozi wa chama zinatokana na imani waliyopewa na chama pamoja na wanachama wake, hivyo hawapaswi kutumia nyadhifa hizo kwa maslahi binafsi au kuruhusu migawanyiko isiyo na tija.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button