Ahoua aitanguliza Simba huko

ZANZIBAR; JEAN Charles Ahoua ameitanguliza Simba tayari huko Zanzibar.

Pengine ndivyo unavyoweza kuzungumzai mchezo kwa kwanza wa nusu fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika kati ya Simba ya Tanzania na Stellenbosch FC ya Afrika Kusini unaofanyika Uwanja wa New Amaan Complex, Zanzibar.

Hivi sasa ni mapumziko, Simba ikiwa mbele kwa bao 1-0 lililofungwa na Ahoua kwa mpira wa adhabu dakika ya 45+2.



