Barcelona yaanza mkakati kumsajili Haaland
TETESI za usajili zinasema klabu ya Barcelona ipo tayari kuanza mkakati kumsajili mshambuliaji wa Manchester City, Erling Haaland mwaka 2026, ikiamini mkataba wake mpya na kampuni ya Nike utaipa fedha kukamilisha dili lenye thamani ya pauni milioni 149.1 mwisho wa msimu ujao.
Kiasi hicho kitamfanya Haaland kuwa mchezaji ghali zaidi katika historia ya Barcelona. (El Nacional – Spain)
Katika hatua nyingine fowadi wa Manchester United Marcus Rashford ana nia kujiunga na Barcelona, lakini klabu hiyo ya Hispania inaona bei ya pauni milioni 40 ni kubwa kuimudu. (The i Paper)
Man Utd inatumaini kumuuza Rashford ili kupata fedha kumsajili winga Rodrygo wa Real Madrid.
Mashetani hao wekundu wanajiandaa kulipa pauni milioni 127.8 kuwashinda wapinzani wake Arsenal, Chelsea, Liverpool na Man City. (TodoFichajes – Spain)
Liverpool inataka kumuuza Diogo Jota kwa ada ya karibu pauni milioni 50.
Aston Villa, Newcastle United na Wolverhampton Wanderers zina nia pamoja na klabu za Saudi Arabia kumsajili mchezaji huyo, huku Liverpool ikitaka kukusanya fedha ili kumsajili wing wa Bayern Munich, Kingsley Coman kwa pauni milioni 34. (CaughtOffside)
Ni Newcastle United inayoongoza mbio kumsajili beki wa kati wa Crystal Palace, Marc Guehi mbele ya Chelsea, Tottenham na Man City. (The Sun)



