Miriam Odemba: Mimi ni chuo mavazi ya heshima

DAR ES SALAAM: “Mimi nipo, njooni kwa Miriam Odemba ili ujifunze namna halisi ya kuvaa mavazi maalum kwa mazingira maalum, na bado upendeze, mimi ni chuo cha mavazi ya heshima,”ameandika mwanamitindo maarufu Miriam Odemba.

SOMA ZAIDI: Miriam Odemba: Mafanikio sio hadhi bali bidii, utu …

Miriam ametoa kauli hiyo kupitia ukurasa wake wa Instagram ukiwa ni ushauri kwa wanawake wanaohusika na sanaa za mavazi na watu maarufu ili kulinda maadili ya kitanzania katika suala la uvaaji.

“Sitozi mtu pesa yoyote ile kuniiga, ila tuu, nitakukataa pale utakaposhindwa kuzingatia na kutunza maadili ya asili yako, mwanamke mrembo, na hii nazungumza na mabinti zangu, tunaofuatilia ulimbwende na ‘umodel’, ‘fasheni na urembo,” amesema Miriam.

SOMA ZAIDI: Basata, MOF waweka mikakati, Miriam aahidi …

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button