Basata, MOF waweka mikakati, Miriam aahidi makubwa

Katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) Dk Kedmon Mapana amekutana na kufanya kikao na wawakilishi viongozi wa Taasisi ya Miriam Odemba Foundation (MOF) taasisi isiyo ya kiserikali inayojikita katika kusaidia mabinti na jamii kuleta mabadiliko chanya na maendeleo.
Katika kikao hicho, Katibu Mtendaji alimpongeza mwanamitindo mashuhuri, Miriam Odemba, kwa mchango wake mkubwa katika kuinua sekta ya ulimbwende na utanashati nchini, sambamba na jitihada zake za kuboresha maisha ya wasichana na jamii kupitia taasisi yake.
Mazungumzo hayo yalilenga kushirikiana katika miradi mbalimbali yenye tija kwa jamii, hasa katika kuwawezesha mabinti ili waweze kufikia ndoto zao na kuchangia maendeleo ya taifa. BASATA imeeleza utayari wake wa kushirikiana na taasisi hiyo ili kuendeleza vipaji na kukuza sekta ya sanaa na mitindo nchini.
Mkurugenzi wa Miriam Odemba Foundation, Miriam Odemba Kwanza ametoa shukrani za dhati kwa Basata kwa kutambua kazi wanayoifanya kupitia taasisi hiyo.
“Shukrani maalum kwa team yangu ,hasa kwa Mkurugenzi Mtendaji wetu, Jennifer Mteleke. Kujitolea kwako ni nguvu inayoendesha dhamira yetu. Na kwa Watanzania wenzangu, msaada wenu na heshima ni kila kitu kwangu. Nisingekuwa hapa leo bila upendo na moyo wa kuhamasisha kutoka kwa watu wangu,” ameeleza Miriam Odemba.
Miriam amesema kuwa ni dhamira yake ya dhati kuleta mitindo ya Tanzania kwenye jukwaa la kimataifa na siyo yeye binafsi bali kuunda fursa kwa kizazi cha sasa na baadaye kilichojaa wabunifu, na wasanii.
“Tanzania ina vipaji ama talanta nyingi, na muda umefika wa kuinua sekta ya mitindo na uanamitindo ya Tanzania hadi viwango vya kimataifa, hasa kwa vijana wa karne hii. Tuko tayari kufungua milango, kujenga uhusiano wa kimataifa, na kubadilisha ndoto kuwa uhalisia,”ameongeza Miriam.
penis enlargement