Biden augua saratani ya tezi dume

WASHINGTON DC: RAIS wa zamani wa Marekani, Joe Biden, amebainika kuugua saratani ya tezi dume, hali ambayo imezua maswali kuhusu afya yake, hasa alipokuwa akihudumu katika Ikulu ya White House.

Taarifa iliyotolewa na ofisi yake Jumapili ilieleza kuwa Biden, mwenye umri wa miaka 82, aligunduliwa na ugonjwa huo Ijumaa baada ya kuonana na daktari kufuatia dalili za matatizo ya njia ya mkojo.

Madaktari wameeleza kushtushwa na kasi ya aina hiyo ya saratani, ambayo tayari imesambaa hadi kwenye mifupa yake, na kushangazwa kwa nini haikugunduliwa mapema.

Hata hivyo, wataalamu wa afya wamesema kuwa baadhi ya saratani huweza kukua haraka bila kuonesha dalili, huku wanaume wengi walio na umri zaidi ya miaka 70 wakiwa hawafanyi uchunguzi wa kiafya mara kwa mara.

Rais wa zamani Donald Trump aliibua mjadala zaidi kwa kudai kuwa Biden alificha taarifa hizo kutoka kwa umma, akisisitiza kuwa ukweli ungewekwa wazi mapema.

SOMA: Biden aliagiza jeshi kusaidia uokoaji Florida

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button