MAREKANI : RAIS wa Marekani amemuru kupelekwa kwa wanajeshi 1,000 kwenye shughuli za uokozi katika jamii zilizoathiriwa na kimbunga Helene kusini mashariki mwa Marekani.
Kwa mujibu wa Ikulu ya Marekani imesema kuwa wanajeshi hao watasaidia katika kupeleka chakula , maji pamoja na bidhaa nyingine muhimu kwa waathirika.
Upelekaji huo pia utaongeza idadi ya maafisa wa uokozi pamoja na kusaidia idara ya kitaifa ya dharura , FEMA na mashirika mengine kufikia watu waliopo kwenye maeneo yalioathiriwa zaidi.
Rais Joe Biden na Makamu wake Kamala Harris wametembelea maeneo kadhaa kuangalia athari zilizoweza kujitokeza kufuatia Kimbunga Helene katika majimbo ya North na South Carolina na Georgia .
SOMA: Mamia ya watu hawajulikani walipo
Kwa sasa majimbo yaliyopo North na South Carolina yamebaki bila huduma muhimu kama umeme na mawasiliano , huku timu za waokoaji zikiendelea kutafuta watu waliotoweka kufuatia kimbunga hicho ambacho tayari kimeua takriban watu 166.
Zaidi ya wakazi milioni 1.2 kufikia jumatano hawakuwa na umeme kwenye majimbo yalioathiwa.