Mamia ya watu hawajulikani walipo

MAREKANI  : WAKAZI wa jimbo la North Carolina  Septemba 30  walikabiliana na uharibifu mkubwa kutokana na kimbunga Helene huku mamia ya watu wakiwa  hawajulikani walipo.

Kimbuga hicho kimeleta madhara makubwa jimboni humo ikiwemo  barabara kusombwa na mafuriko pamoja na ukosefu wa huduma muhimu.

Zaidi ya vifo 100 vimeripotiwa kwenye zaidi ya majimbo 6 kusini mashariki mwa Marekani kutokana na kimbunga hicho kilichoanzia kwenye kaunti ya Big Bend, Florida Septemba 26,Jioni kabla ya kuendelea kwenye majimbo ya Georgia na South na North Carolina.

Advertisement

Mshauri wa wizara ya Usalama wa ndani wa Marekani, Liz Sherwood Randall, alisema huko White House kuwa hadi watu 600 bado hawajulikani walipo ingawa idadi hiyo huenda ikapungua kadri timu za uokozi zinavyofika maeneo ya ndani.

SOMA :Waliokufa kimbunga Marekani wafikia 26