Simba watafuna kiporo cha Singida

DAR ES SALAAM; MAMBO yanazidi kuwa matamu kwa Simba kwenye Ligi Kuu Tanzania Bara baada ya leo kushinda bao 1-0 mchezo wake wa kiporo dhidi ya Singida Black Stars Uwanja wa KMC, Dar es Salaam, mfungaji akiwa Steven Mukwala.

Kutokana na ushindi huo Simba sasa imefikisha pointi 72 ikiendelea kushika nafasi ya pili nyuma ya Yanga inayoongoza ikiwa na pointi 73, zote zikiwa zimecheza michezo 27.




