Mkutano Mkuu CCM kuanza leo

MKUTANO Mkuu Maalumu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) unaanza leo Dodoma.

Mkutano huo unatarajiwa kuhudhuriwa na wajumbe takribani 2,000 katika ukumbi wa Jakaya Kikwete jijini Dodoma.

Mkutano huo unatajiwa kuwa na ajenda tatu ikiwamo ya uzinduzi wa Ilani ya Uchaguzi wa chama hicho 2025/2030.

Pia, wajumbe watakuwa na kazi ya kupokea na kujadili utekelezaji wa Ilani za uchaguzi ya mwaka 2020 hadi 2025 wa serikali zote mbili ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ).

Ajenda nyingine katika mkutano ni mabadiliko madogo ya Katiba ya chama hicho.

Mkutano huo umetanguliwa na kikao cha Kamati Kuu ya CCM kilichofanyika Ikulu Chamwino mkoani humo Mei 27 kikiongozwa na Mwenyekiti wa CCM Taifa, Rais Samia Suluhu Hassan.

Kkao hicho kilifuatiwa na kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM kitachofanyika Dodoma Mei 28 katika Ukumbi wa NEC uliopo kwenye jengo la White House jijini Dodoma.

Januari 18, mwaka huu CCM ilifanya Mkutano Mkuu wa CCM jijini Dodoma na wajumbe waliwapitisha kwa kauli moja Rais Samia kuipeperusha bendera ya chama hicho katika Uchaguzi Mkuu utakaofanyika Oktoba mwaka huu.

Pia, mkutano huo ulimpitisha Katibu Mkuu wa chama hicho, Balozi Dk Emmanuel Nchimbi awe mgombea
mwenza wa CCM na Stephen Wassira kuwa Makamu Mwenyekiti wa chama hicho Tanzania Bara akichukua
nafasi ya aliyekuwa Makamu Mwenyekiti, Abdulrahman Kinana aliyeng’atuka nafasi hiyo.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button