Mwisho wa majigambo Ulaya leo

FAINALI ya kibabe ya michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya (UCL) kati ya Paris Saint-Germain (PSG) ya Ufaransa na Inter Milan ya Italia inafanyika leo kwenye uwanja wa Allianz uliopo jiji la Munich, Ujerumani.
Mchezo huo utaamuliwa na pilato Istvan Kovacs kutoka Romania.
Kutinga fainali, PSG imetoa Arsenal katika nusu fainali kwa jumla ya mabao 2-1 wakati Inter imeitoa Barcelona kwa jumla ya mabao 4-3.
Michuano hiyo ya Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu wa 2024/2025 iliendeshwa kwa mfumo wa ligi ikijumuisha timu 36.
Matengwa watetezi ilikuwa ni Real Madrid iliyotolewa na Arsenal katika hatua ya robo fainali kwa jumla ya mabao 5-1.



