Samia achangia mil 150/- ujenzi kituo cha watoto
RAIS Samia Suluhu Hassan amechangia sh milioni 150, kwa ajili ya ujenzi wa Kituo cha Watoto wenye mahitaji maalumu wenye usonji kinachotarajiwa kujengwa na Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania(KKKT) Dayosisi ya Mashariki na Pwani mkoani Pwani.
Kituo hicho kiitwacho Bagamoyo Diaconic Lutheran Centre kinatarajiwa kujengwa wilaya ya Bagamoyo.
Katika Harambee hiyo, washauri wa Rais wamechangia shs milioni 100, hivyo kufanya ofisi ya Rais kuchangia shs milioni 250 kwa ajili ya ujenzi wa kituo hicho.

“Kiwango nilichojiwekea kuchangia katika shughuli za kanisa ni shs milioni 100, lakini nikivaa kofia ya bibi nitachangia shs milioni 50, na wasaidizi wangu wamejichanga na kuchangia shs milioni 250, hivyo kama ofisi yangu tunachangia shs milioni 250,” amesema Rais Samia.
Akizungumza katika Harambee hiyo Rais Samia amemhakikishia Mkuu wa Kanisa hilo kuwa serikali itaendelea kushirikiana bega kwa bega katika hatua zote za ujenzi pamoja na uendeshaji wa kituo hicho.

“Nasimama mbele yenu kama mama ambaye nabeba dhamana ya malezi kama mama, situ wa mahaitaji maalumu bali wote, ninasimama nikiwa naelewa fika jukumu kubwa wanalolibeba akina mama wanapokuwa na watoto wenye uhitaji maalumu,” amesema.
Aidha, Rais Samia ameahidi kuwepo katika uzinduzi wa kituo hicho kuona matokeo ya tulio lilofanyika leo.
Katika harambee hiyo wadau mablimabli wametoa ahadi zao, miongoni mwao ni Shirika la Nyumba la Taifa shs milioni 10, NBC Bank shs milioni 50, Ofisi ya Mkoa wa Dar es Salaam shs milioni 20, Maendeleo bank shs milioni 140, TANESCO shs milioni 20, NMB Bank shs milioni 50, CRDB Bank shs milioni 100, CRDB Bank Insurance shs milioni 10, CRDB Bank Foundation shs milioni 50 na Chuo Kikuu cha Tumaini Dar es Salam shs milioni 10.

Mkuu wa KKKT Askofu Dk Alex Gehaz Malasusa amemshukuru Rais Samia kwa mchango wake na uwepo wake katika harambee hiyo akisema unaleta ujumbe kwamba walemavu ni sehemu ya taifa na wanahaki ya elimu na kujifunza.
Amesema tayari kanisa hilo limeanza michoro ya usanifu wa majengo na imekamilika, huku ikikusanya bilioni 2.7/- kupitia harambeee ya ndani iliyojumuisha sharika na mitaa mbalimbali.



