Dk Mpango akutana na Waziri wa Mazingira wa Sweden

MAKAMU wa Rais Dk Philip Mpango amekutana na kufanya mazungumzo na Waziri na Mazingira na Hali ya Hewa wa Sweden, Romina Pourmokhtari kando ya Mkutano wa Tatu wa Umoja wa Mataifa kuhusu Bahari unaofanyika jijini Nice, Ufaransa.

Mazungumzo hayo yamelenga kuongeza ushirikiano baina ya Tanzania na Sweden katika kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi, kubadilishana maarifa katika kilimo janja, kuhamisha teknolojia za kisasa za kulinda mazingira pamoja na matumizi ya nishati safi ya kupikia.



