Usajili bodaboda, leseni za bajaji, guta wapunguzwa

DODOMA; SERIKALI inakusudia kufanya marekebisho kwenye Kanuni za Sheria ya Usalama Barabarani za mwaka 2024 ili kupunguza ada ya usajili wa pikipiki za biashara (bodaboda) na kupunguza ada ya leseni ya uendeshaji wa pikipiki, guta na bajaji.

Kauli hiyo imetolewa na Waziri wa Fedha, Dk Mwiguku Nchemba, wakati anawasilisha makadirio ya mapato na matumizi ya Serikali kwa mwaka 2025/26 bungeni leo Juni 12, 2025.

-Napendekeza kufanya marekebisho kwenye Kanuni za Sheria ya Usalama Barabarani za mwaka 2024 kama ifuatavyo: Kupunguza ada ya usajili wa pikipiki za biashara kutoka shilingi 340,000 hadi shilingi 170,000 kwa miaka mitatu. Ada husika italipwa wakati wa usajili wa awali pekee.

“Kufuta kodi ya mapato kwa mwaka inayolipwa kwa utaratibu wa presumptive tax na kuanzisha ulipaji wa mara moja wa ada na presumptive tax kwa kiasi cha shilingi 120,000 badala ya shilingi 290,000.

“ Ada na kodi hii italipwa wakati wa usajili; na Kupunguza ada ya leseni ya uendeshaji wa pikipiki, bajaji na guta kutoka shilingi 70,000 hadi shilingi 30,000,” amesema Waziri Nchemba.

 

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button