Serikali yawasilisha bajeti ya Sh tril. 56

DODOMA; Waziri wa Fedha, Dk Mwigulu Nchemba, amewasilisha makadirio ya mapato na matumizi ya Serikali ya shilingi trilioni 56.49 kwa mwaka 2025/26 .

β€œMakadirio ya matumizi ya Serikali ya shilingi trilioni 56.49 kwa mwaka 2025/26 yanajumuisha: Stahiki za watumishi na michango ya pensheni (Serikali Kuu) shilingi trilioni 9.17;

β€œUnunuzi wa bidhaa na huduma shilingi trilioni 5.58; malipo ya riba za mikopo shilingi trilioni 6.49; na ruzuku (subsidies & transfers) kwa taasisi za Serikali, mashirika ya umma na Mamlaka za Serikali za Mitaa shilingi trilioni 22.17.

β€œAidha, Serikali inatarajia kutumia shilingi trilioni 7.72 kugharamia malipo ya mtaji kwa deni la ndani na nje,” amesema Waziri Nchemba.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button