CTIDO mabingwa wa ligi wilaya Arusha

ARUSHA: TIMU ya CTIDO imefanikiwa kutwaa ubingwa wa ligi ya Wilaya ya Arusha baada ya kuisambaratisha timu ya Uhasibu Academy kwa jumla ya magoli 2-1 katika mchezo wa fainalo uliochezwa uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini hapa.
Mchezo huo ulihudhuriwa na Mkuu wa Wilaya ya Arusha, Joseph Modest Mkude ambaye alikabidhi kombe la ubingwa wa ligi hiyo kwa mabingwa hao.

Ligi ya Wilaya ya Arusha ilihusisha timu 12 za vijana walio na umri chini ya miaka 17 ambazo ni Arydo Academy,Black eagle ,Nyota academy, Peace academy, Satino academy,OB fc, CTIDO, Uhasibu, Magnet, Arabic, FSA academy ,KYVF academy.



