Mnyama yupo bwana!

DAR ES SALAAM; HATIMAYE Simba imewapa faraja mashabiki wa mpira waliokuwa na hofu kuhusu mchezo wa leo Ligi Kuu Tanzania Bara kati yao na Yanga.

Tangu Bodi ya Ligi (TPLB), itangaze tarehe ya mchezo huo, Simba haikuweka chochote kwenye mitandao ya kijamii kuhusu mchezo huo, hali iliyozua sintofahamu kama wataingiza timu na hadi jana Simba walishindwa kutokea kwenye mkutano wa kiufundi na waandishi wa habari.

Lakini mchana huu ukurasa rasmi wa Simba umepambwa na picha ya nahodha wa timu hiyo Mohammed Hussein na unazungumzia mchezo huo wa mwisho kwenye Ligi Kuu Tanzania Bara msimu wa mwaka 2024/25.

 

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button