Upotevu wa nafaka wapungua hadi asilima 20

DAR ES SALAAM: OFISA Kilimo Mkuu kutoka Wizara ya Kilimo, Magreth Natai amesema wamefanikiwa kupunguza upotevu wa mazao ya nafaka kutoka asilimia 30 hadi 20 lengo ni kufikia asilimia tano.

Akizungumza katika Maonesho ya 49 ya Kimataifa ya Biashara Sabasaba, Natai amesema kwenye eneo la upotevu wa mazao wizara imejikita kwenye ujenzi wa maghala nchi nzima ambapo wana maghala makubwa ya uhifadhi wa chakula na pia katika maonesho wanatoa elimu hiyo.

“Katika kaya tumekuwa tukitoa elimu katika mchakato wa uhifadhi kuanzi kuvuna jinsi gani ya kuanika mazao yakauke, kuepuka sumu kuvu na wanapata mafunzo kupitia maafisa kilimo walioko katika halmashauri,” amesema Natai.

Amesema wamekuwa na ujenzi wa maghala katika ngazi ya kijamii yaani kwenye halmashauri  na wamekuwa wakijenga kila mwaka  wakishirikiana  na wadau binafsi.

“Haya yamesaidia kudhibiti upotevu ,tuna teknolojia za uhifadhi ambazo hazitumii kemikali yoyote na mkulima akielimishwa hatatumia kemikali,”amesisitiza Natai.

Katika maonesho hayo amesema wakulima wengi  wamekuwa wakiulizia mbegu na zana za kilimo na  kumekuwa na mwamko wa kutumia mbegu bora na takribani ya zaidi ya miaka 10 nchi imekuwa ikijitosheleza kwa chakula zaidi ya asilimia 100.

“Mwaka huu tuna utoshelevu wa asilimia 128 nani kutokana na huduma kuboreshwa kama huduma za ugani ,mbegu,dawa,vifaa vya kilimo na wengi wanahamasika kufanya kilimo cha kisasa na pia uwekezaji umekuwa mkubwa.

Amefafanua kuwa katika maonesho hayo wizara ya kilimo ipo na taasisi na bodi mbalimbali kama bodi ya Kahawa,Mkonge,Chai,Tumbaku na mazao yote  na taasisi  kama TARI inayohusika na utafiti,TOSI inahusika na ubora wa mbegu na ASA wanaoshughulika na mbegu.

“Kuna taasisi na bodi 21 katika mabanda yetu tunataka wananchi wafike hapa na wajifunze mambo mengi watapata taarifa mbalimbali,vifaa vya kilimo viko hapa lakini vilevile watajifunza wizara inafanya nini katika bodi zake.

Ameongeza “Tunawakaribisha sana wananchi waweze kushiriki na tunajua wizara ya kilimo inajukumu la kulinda usalama wa chakula na lishe tumejipanga vizuri na tumejiwekea malengo kuhakikisha tunafiki.

Amebainisha mikakati yao kuwa ni kuhakikisha kinachozalishwa hakipotei ,kuongeza umwagiliaji,mfumo ya taarifa za wizara pia unavipeperushi vya kuwapatia wakulima waweze kusoma na kama watahitaji maelezo zaidi watapiga simu.

Kwa upande wake Mkulima Fransic Osman amesema yeye  analima ufuta kwa mkoa wa Pwani ambapo tangu ameanza kulima kwa mwaka mmoja anaweza kupata tani 30 hadi 15 kutokana na msimu.

“Natarajia kupanda miche isiyopungua 400 lakini pale SUA wanauza mche mmoja Sh 2000 na mche mmoja una maembe 1000 ukiuza kwa bei ya jumla kwa Sh 500 kwa msimu mmoja hukosi Milioni 10.

Amependekeza wizara kuwapa  dawa za kuua wadudu,dawa za magugu wasije  wakapata hasara kama ilivyotokea 2022 ambapo  walipuliza dawa na  haikufanya kazi kama inavyotakiwa.

‘Nishauri wapite katika maeneo ya wakulima na wafanye sensa ya wakulima wakitoa ruzuku inakuwa rahisi kumfikia mkulima.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button