Timu ya Mabingwa wa Safari Lager yatangazwa

DAR ES SALAAM: Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) imetangaza wachezaji 22 watakaoiwakilisha timu ya Mabingwa wa Safari Lager 2025.

Wachezaji hao walichaguliwa kupitia mchakato wa kutafuta vipaji katika mikoa ya Mbeya, Arusha, Mwanza na Dar es Salaam.

Timu hiyo itakutana na Yanga katika fainali ya Kombe la Safari Lager Julai 26 mwaka huu Uwanja wa KMC Mwenge na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Profesa Palamagamba Kabudi anatarajiwa kuwa mgeni rasmi.

Kombe la Safari Lager lilianzishwa 2024 likiwa na lengo la kuibua na kuinua vipaji vya soka vya vijana nje ya mfumo wa klabu na yalikuwa kwa wachezaji wenye umri kati ya miaka 18 hadi 24 chini ya usimamizi wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF).

Khensani Mkhombo, Mkuu wa Masoko wa TBL, alisema kuwa mpango huu ulilenga kubadilisha mfumo wa kugundua vipaji vya soka nchini.

“Lengo letu katika Kombe la Safari Lager tulitaka kuunda tukio litakalobadili namna vipaji vya soka vinavyogunduliwa na kusherehekewa. Vijana hawa hawakusajiliwa ila walionekana na makocha, mashabiki na jamii zao”

Kikosi kilichochaguliwa ni makipa Edward Mjanja (Arusha) na Lupakisyo Mwakyando (Dar es Salaam).

Mabeki ni Seleman Mangoma (Dar es Salaam), Sadala Sabula (Mbeya), Abdoun Ibrahim (Dar es Salaam), Paul Kona (Mwanza), Ally Manzi (Arusha), Rashidi Fumbwe (Dar es Salaam), Izirael Lyimo (Arusha) na Japhet Gabriel (Mbeya)

Viungo ni Yasin Chondi (Dar es Salaam), Mickdady Mgeta (Arusha), David Kombe (Mwanza), Mahenga Komakoma (Mwanza), Robert Mwakyeja (Mbeya), Godfrey Kapira (Mbeya), Adam Shingini (Mbeya) na Herry Sanga (Mbeya) Washambuliaji ni Petro Paul (Mbeya), Said Bakari (Mbeya), Maximilian Kasisi (Mbeya) na Paschal Elias (Mwanza)

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button