Watu 1,000 kushiriki Mbio za Nyuki kesho

ARUSHA: Msimu wa pili wa mbio za Nyuki Marathon unatarajia kuvuta zaidi ya washiriki 1000 ambao watakimbia Jumapiĺi hii katika viwanja vya AICC Club vilivyopo Kijenge, jijini Arusha.

Hatua hiyo ni kukuza tasnia ya ufugaji nyuki na kumuenzi mdudu nyuki kwa mchango anaoutoa mbio zitakazofanyika Arusha.

Mbio hizo ni maandalizi kuelekea mkutano wa 50 wa Shirikisho la Kimataifa la Vyama vya wafugaji wa nyuki (Apimondia) utakaofanyikia Tanzania kwa mara ya kwanza mwaka 2027 na zitahusisha Kilometa 21,kilometa 10 na kilometa 5.

Wakizungumza na waandishi wa habari kuelekea mbio hizo waandaaji wa mbio,
Ally Saburi ambaye ni Ofisa Mtendaji Mkuu pamoja na Restituta Lopes ambaye ni mwenyekiti wote kutoka Shirika la Worker Bees Africa wameeleza kuwa mbali na kukimbia wananchi watapata na fursa zilizopo kwenye masuala mazima ya ufugaji nyuki.

” Lengo sio kuandaa tu mbio bali ni harakati katika kukuza tasnia ya ufugaji nyuki na ni daraja la kuwaunganisha wafugaji nyuki na wasio wafugaji nyuki pia vijana wapate uelewa na waone ufugaji nyuki ni fursa,” wameeleza waandaaji hao kutoka shirika la workers bees Africa.

Naye Profesa Dosantos Silayo ambaye ni Kamishna wa wa huduma za misitu Tanzania (TFS) pia mwenyekiti wa kamati ya maandalizi ya mkutano wa 50 Apimondia amesema mbizo hizo ni katika kuhamasisha jamii kujiandaa kama nchi kuwa mwenyeji wa mkutano huo wa dunia mwaka 2027 .

“Mbio hizi zinawaleta mataifa mbalimbali pamoja wakiwa wote wanazungumza lugha moja ya kuhifadhi nyuki na kuhamasisha uhifadhi kwa ujumla na kufanya nyuki kuwa moja ya sekta ya kukuza uchumi wa mtu mmoja mmoja na taifa kwa ujumla, hivyo wapenda kichezo wote wajitokeze kwa wingi “,amesema Prof.Silayo.

Kwa upande wake Rais wa Apimondia duniani Dk Jeff Pettis kuna umuhimu mkubwa wa kuendelea kutunza na kufanya udhalishani wa Nyuki kwani ni chanzo cha kuwainua na kuwawezesha vijana kiuchumi, kadhalika ajira hivyo Nyuki Marathoni ni katika kufikisha ujumbe kuhusu uhifadhi Nyuki na udhalishaji wa asali kwa ujumla .

Aidha Mbio hizo zitahudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Apimondia duniani waliongozwa na Rais wake, Apimondia, Makamu wa Rais, Katibu mkuu wa Apimondia bila kusahau viongozi wa Afrika wa shirkisho hilo.

Kwa upande wake katibu wa Chama cha Riadha mkoa wa Arusha, Rogath Steven amesema mbio hizo zimekuwa chachu katika kuibua vipaji vya wanariadha wanaochipukia kadhalika jamii kukifunza na kupata uelewa zaidi wa juu ya uhifahi nyuki na faida zake.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button