Waziri ajiuzulu kuwadharau wananchi

CUBA : WAZIRI wa Kazi wa Cuba, Marta Elena Feitó Cabrera, amejiuzulu kufuatia ukosoaji mkali alioupata baada ya kudai kuwa hakuna ombaomba nchini humo.

Akizungumza katika kikao cha Bunge la Kitaifa, Feitó alisema watu wanaochakura kwenye takataka wanatafuta “pesa rahisi”, kauli iliyozua hasira miongoni mwa raia na viongozi, akiwemo Rais Miguel Díaz-Canel.

Maoni hayo yalionekana kupuuza hali halisi ya maisha ya Wacuba wengi wanaokabiliwa na umaskini mkubwa na uhaba wa chakula. Mwanauchumi Pedro Monreal alijibu vikali kupitia mtandao wa X, akiandika: “Lazima kuna watu pia waliojificha kama ‘mawaziri'”, akionyesha kukerwa na matamshi hayo ya Waziri huyo wa zamani.

Wanaharakati na wasomi kadhaa wa Cuba walijitokeza hadharani wakimtaka Feitó ajiuzulu, wakisema kauli zake ni tusi kwa watu wa Cuba. SOMA: Watafiti Cuba wafanya ziara Serengeti

Shinikizo hilo pamoja na lawama kutoka kwa wananchi ndani na nje ya nchi, hatimaye lilimlazimu kutangaza kujiuzulu kwake wiki hii.

 

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button