Watafiti Cuba wafanya ziara Serengeti

ZIARA ya kikazi ya watafiti wa mimea vamizi kutoka Jamhuri ya Cuba walioungana na wataalamu wa ikolojia kutoka Wizara ya Maliasili na Utalii katika Hifadhi ya Taifa Serengeti inata rajiwa kuwa neema kwa wanyamapori kwenye hifadhi hiyo.

Akizungumza na wata fiti hao katika hifadhi hiyo, Mkuu wa Hifadhi ya Taifa Serengeti, Stephano Msumi alisema wanyamapori hao sasa wataongezewa malisho.

Msumi ameushukuru na kuupongeza uongozi wa Wizara ya Maliasili na Utalii kwa kuwakutanisha watafiti wa wizara hiyo na kutoka nchi ya Cuba kutembelea Hifadhi ya Serengeti.

Alisema hifadhi hiyo ni moja ya hifadhi za taifa zinazochangia kwa kiasi kikubwa katika pato la taifa kupitia utalii hivyo jitihada zinazofanywa na serikali katika kuhakikisha wanya mapori wanapata malisho ya kutosha ni za kuungwa mkono.

Msumi alisema kuna juhudi zinazofanywa na wataalamu kutoka katika hifadhi hiyo za kupambana na mimea vamizi lakini bado hazijazaa matunda yaliyo tarajiwa, hivyo ziara hiyo ni hatua muhimu kufikia malengo.

Mtaalamu mtambuzi wa mimea asili kutoka Cuba, Dk Ramona Oviedo Prieto alishauri wataalamu wa ikolojia wa Hifadhi ya Taifa Serengeti wachukue hatua za haraka za kulinda kingo za Mto Mara uliopo ndani ya hifadhi hiyo kurejeresha mimea ya asili iliyokuwepo pembezoni mwa mto huo.

Wakiwa hifadhini, timu hiyo ya watafiti walitembelea maeneo ya Seronera, Ikoma, Mto Mara na Machochwe na kushuhudia mimea vamizi aina ya gugu karoti ambayo ndiyo imeanza kusambaa kwenye maeneo hayo.

Habari Zifananazo

One Comment

  1. Pata pesa taslimu kila wiki kutoka kwa starehe ya nyumba yako! Fursa hii rahisi ya muda ni kamili kwa mtu yeyote anayetafuta kutengeneza Dola 300-1300 kila wiki. Anza sasa na upokee malipo yako ya kwanza baada ya siku chache. Usikose – jiunge leo. Gonga Uchumi wa Fedha AU Uwekezaji.
    Hivi ndivyo ninavyofanya…………………….. BOFYA http://Www.WorksProfit7.Com

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button