Bunge lapigwa stop kumuondoa Sara Duterte

MANILA : MAHAKAMA ya Juu nchini Ufilipino imetupilia mbali uamuzi wa bunge wa kumuondoa madarakani Makamu wa Rais Sara Duterte, ikisema mchakato huo ulikuwa kinyume cha katiba.
Bunge lilimng’oa madarakani mwezi Februari kwa tuhuma za kutumia vibaya fedha za umma, kujilimbikizia utajiri na kutoa vitisho vya kumuua Rais Ferdinand Marcos Jr, mkewe na Spika wa Bunge.
Hata hivyo, Mahakama imesisitiza kuwa uamuzi huo haumaanishi kuondolewa kwa mashitaka yanayomkabili makamu huyo wa rais. SOMA: Zanzibar, ufilipino kushirikiana ‘uchumi wa buluu’
Sara Duterte, ambaye ni binti wa rais wa zamani Rodrigo Duterte anayekabiliwa na mashitaka ya uhalifu dhidi ya ubinadamu katika Mahakama ya Kimataifa ya ICC, anaonekana kuwa mgombea mwenye nguvu katika uchaguzi wa urais wa 2028, ambao Marcos hataruhusiwa kushiriki kutokana na kizuizi cha muhula mmoja.



