Zanzibar, ufilipino kushirikiana ‘uchumi wa buluu’

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi amesema Zanzibar ina mengi ya kujifunza uzoefu na weledi kutoka nchi ya Ufilipino hasa kwenye sekta za mafuta na gasi ,afya, utalii na uvuvi.

Dk. Mwinyi aliyasema hayo leo tarehe 02 Machi, 2023 Ikulu Zanzibar alipokutana na Balozi wa Ufilipino Tanzania ,Marie Charlotte G.Tang aliyefika ikulu hapo kujitambulisha.

Dk. Mwinyi amemuomba Balozi wa Ufilipino kuitangaza Zanzibar katika fursa mbalimbali ambazo zinapatikana visiwa humo.

Balozi Marie Charlotte G.Tang amesema ataongeza uhusiano kati ya Ufilipino na Tanzania pia amekubali kuitangaza na kuwashawishi wawekezaji kutoka nchini mwake kuja Zanzibar kuangalia fursa za Uwekezaji zinazopatikana kutokana na kufanana mazingira kati ya Ufilipino na Zanzibar.

Habari Zifananazo

Back to top button