Wizara yajivunia taswira, heshima ya Tanzania kimataifa
DODOMA; WIZARA ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, imesema kufuatia utekelezaji wa vipaumbele vya wizara na kwa kuzingatia Malengo ya Kimkakati ya Sera ya Mambo ya Nje ya Mwaka 2001, Toleo la Mwaka 2024, mafanikio mbalimbali yamepatikana.
Kauli hiyo imetolewa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Mahmoud Thabit Kombo, Balozi Kombo leo Mei 26, 2026 alipokuwa akiwasilisha makadirio ya mapato na matumizi ya wizara hiyo kwa Mwaka wa Fedha 2026/27.
“Kwa muhtasari mafanikio hayo ni kama ifuatavyo: Kuimarika kwa taswira na heshima ya Taifa letu katika nyanja za kimataifa;
“Kuimarika kwa ushirikiano wa uwili ikiwemo kufanikisha upatikanaji wa rasilimali fedha, ujuzi na teknolojia kutoka nchi rafiki na fursa zitokanazo na Mikataba na Hati za Makubaliano zilizosainiwa;
“Kuimarika kwa ushirikiano wa kikanda hususan kupitia utekelezaji wa Itifaki na Programu za Mtangamano zenye maslahi ya kiuchumi, kisiasa na kijamii kwa Taifa letu;
“Kuimarika kwa ushirikiano wa kimataifa, ikiwemo kuwezesha ushiriki wa Tanzania katika ajenda zinazohitaji juhudi za pamoja kama vile masuala ya mazingira, mabadiliko ya tabianchi, nishati safi ya kupikia hususan kwa kinamama, kupambana na magonjwa ya mlipuko na uhalifu unaovuka mipaka,” amesema Waziri Kombo.
Ametaja mafanikio mengine ni kuwezesha Tanzania kupata nafasi za kimkakati katika jumuiya za kikanda na Kimataifa ikiwemo uteuzi wa Rais Samia Suluhu Hassan, kushika nafasi ya Makamu Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika; Dk Jakaya Kikwete, Rais Mstaafu wa Tanzania kwa nafasi ya Mwakilishi wa Ngazi ya Juu wa Mwenyekiti wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika katika eneo la Pembe ya Afrika na Bahari ya Shamu na Balozi Stephen Mbundi kuwa Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.
“Kuimarika kwa mchango wa Watanzania waishio nje ya nchi na raia wa nchi nyingine wenye asili ya Tanzania katika maendeleo ya Taifa hususan katika sekta za fedha, uwekezaji, nyumba, kilimo na viwanda,” amesema Waziri Kombo na kuongeza”.
“Kulinda usalama wa Watanzania walio nje ya nchi na kuwarejesha nyumbani salama kutoka kwenye maeneo yaliyokumbwa na vita na machafuko;
“Kuimarika kwa utoaji wa elimu kwa umma hususan utekelezaji wa Sera ya Mambo ya Nje ya Mwaka 2001, Toleo la Mwaka 2024 kupitia vyombo vya habari, mitandao ya kijamii, machapisho na njia za kidijitali;
“Kuimarika kwa mazingira ya utendaji kazi kwa kufanikisha uendelezaji wa milki ikiwemo ukarabati wa ofisi na makazi ya watumishi katika Balozi za Tanzania Nje; na Kuanza kwa utekelezaji wa mradi wa kimkakati wa ujenzi wa kituo kipya na cha kisasa cha Mikutano cha Mlima Kilimanjaro (Mt. Kilimanjaro International Convention Centre- MK-ICC),” amesema.




Fastest Casino Withdrawl matters to players who want smooth control of their winnings after a positive session. A
strong withdrawal process should feel simple, from thhe first
cashout request to the final payment confirmation.
Before playing, it is useful to compare payout limits, processing
times, accepted payment methods, possible fees, and
account verification rules.
Speedd becomes even more valuable when the cashier is easy too use and every step is explained
without confusion. Players can often avoid delays by keeping personal details accurate,
completing checks early, and reading bonus terms before requestin a withdrawal.
Actie promotions may affect when funds are available, so clear rules are
important. With trusted payment tools, the fastest
casino withdrawal experience can add comfort to online
entertainment.