Malori 120 ya msaada yaingia Gaza

JERUSALEM: SERIKALI ya Israel imesema zaidi ya malori 120 ya msaada wa chakula yamesambazwa katika Ukanda wa Gaza na Umoja wa Mataifa pamoja na mashirika ya misaada, ikiwa ni siku ya kwanza ya kusitishwa kwa muda kwa mapigano.
Mamlaka ya Israel inayoshughulikia Masuala ya Palestina (COGAT) ilithibitisha kupitia chapisho kwenye mtandao wa X kwamba misaada hiyo imeingizwa Gaza kwa usalama.
Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu, amepuuzilia mbali madai kuwa nchi yake inatumia njaa kama silaha ya vita dhidi ya Hamas, akisema kuwa madai hayo ni uongo mkubwa.
Amesisitiza kuwa hakuna sera ya njaa Gaza na kwamba tangu kuanza kwa vita, Israel imekuwa ikiruhusu na kuwezesha misaada ya chakula kuingia katika eneo hilo.
Aidha, Israel ilitangaza kusitisha kimkakati operesheni zake za kijeshi Gaza na kuahidi kufungua njia salama kwa ajili ya misaada, ikiyataka mashirika ya misaada kuongeza kasi ya usambazaji wa chakula kwa wakazi wa Gaza. SOMA: Rwanda yapeleka msaada wa kibinadamu Gaza



