Kasharunga FC yatwaa ubingwa Miamia Cup

MULEBA: Timu ya Kasharunga FC imetwaa ubingwa na kujishindia kitita cha Sh milioni 10 baada ya ushindi dhidi ya Muhalila Cup All Stars kwa mikwaju ya penati 6-5 katika mashindano ya kombe la Miamia yaliyofanyika wilayani Muleba.
Michuano ya MiaMia imehitimishwa kwa msimu wa 9 ambapo timu ya Muhalila Cup All Starts imejinyakulia Sh Milioni 5 kama mshindi wa pili.
Mwandaaji wa nashindano hayo Sadath Yahya alisema kuwa mashindano hayo yamekuwa chachu kwa vijana kuonyesha vipaji kwa miaka 9 mfululizo huku wadau wanaotoa elimu ya Sheria na wafanya biashara wakiyatumia mashindano hayo kama fursa ya kutangaza huduma zao kwa wananchi
Alisema kuwa michuano hiyo ambayo imedumu mwezi mmoja ilizishirikisha timu 16 huku timu zote zilizoingia kuanzia robo fainali zikijipatia Milioni moja moja na ambazo ziliishia makundi wakipata Jezi na mpira.

Moja ya changamoto ambayo ameitaja kama Mdau wa michezo ni uwepo wa viwanja vichache Ambavyo havikidhi mahitaji ya vijana wanaotaka kuonyesha vipaji katika wilaya hiyo.
Mdau wa michezo katika wilaya ya Muleba Fortunas Muhalila ambaye pia amekuwa akiandaa michuano ya Muhalila Cup alisema kuwa wilaya hiyo unakimbwa na changamoto ya viwanja jambo ambalo linafifisha vipaji vya wachezaji
Alisema serikali kwa kushirikiana na wadau wote wa maendeleo wakiweka nguvu katika michezo huenda wilaya hiyo itazalisha vipaji halisi ambavyo vitaonekana kitaifa na kimataifa huku akipongeza Ubunifu wa wadau kuendelea Kuanzisha mashindano ya mpira wa miguu katika wilaya ya Muleba
Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Muleba Issaya Mbenje amepongeza ushiriki wa vijana katika fursa mbalimbali za wadau wanajitokeza Kuandaa mashindano ya michezo
Alisema kuwa tayari Halmashauri ya Wilaya ya Muleba imebaini maeneo sita kwa ajili ya kutengeneza viwanja vya michezo mbalimbali ambapo kwa mwaka huu wa fedha wametenga fedha kwa ajili ya kuanza utengenezaji ili vijana wapate sehemu salama ya kuoneshea na kuendelezea vipaji vyao
“Zamani ilikuwa ngumu kupata timu ya kutuwakilisha katika mashindano ya mkoa lakini sasa tunashukuru wadau kwa kuendelea kuibia fursa za michezo na Kubaini vipaji vya vijana na sisi kama serikali tutakuwa na ninyi bega kwa bega katika maandalizi yote ya michezo na tutatatua changamoto za viwanja vya kuchezea”alisema Mbenje
Mdhamini mkuu wa mashindayo hayo kutoka shirika la msaada wa kisheria la muhola Sauro Marahuri alisema mashindano hayo yamekuwa yakitumika kuhamisha jamii kuachana na vitendo vya kikatili na kuwapatia wananchi huduma za msaada wa kisheria.



