Mahakama yamkuta Uribe na hatia

BOGOTA : RAIS wa zamani wa Colombia, Alvaro Uribe, amepatikana na hatia ya kujaribu kuwarubuni mashahidi katika kesi ya ufisadi inayomkabili.

Hukumu hiyo imetolewa mjini Bogota baada ya kesi iliyodumu kwa miezi sita, ambapo waendesha mashtaka waliwasilisha ushahidi kuwa Uribe alijaribu kuwahonga mashahidi waliomtuhumu kuwa na uhusiano na kundi la wanamgambo katika miaka ya 1990.

Uribe (73), ambaye alitawala kati ya mwaka 2002 hadi 2010 akiungwa mkono na Marekani, anakabiliwa na kifungo cha hadi miaka 12 jela, ingawa adhabu yake itatolewa katika kikao kingine cha mahakama.

Mwanasiasa huyo wa kihafidhina anabaki kuwa kiongozi mwenye mgawanyiko mkubwa nchini Colombia, akipendwa na baadhi kwa kuimarisha usalama wa taifa na kuchukiwa na wengine kwa tuhuma za ukiukwaji wa haki za binadamu na uhusiano wake na makundi yenye silaha. SOMA: Rais wa Shirikisho la Soka Colombia akamatwa

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button