Tetemeko la kihistoria laleta taharuki Urusi

MOSCOW, URUSI : TETEMEKO kubwa la ardhi lenye ukubwa wa 8.7 kwenye kipimo cha Richter limeripotiwa mapema leo nchini Urusi katika Rasi ya Kamchatka, na kusababisha tahadhari ya tsunami kwa nchi kadhaa, zikiwemo Japan, Alaska na Hawaii.
Tukio hilo linatajwa kuwa tetemeko kubwa zaidi halikuwahi kutokea katika eneo hilo tangu mwaka 1952. Kwa mujibu wa Mamlaka ya Jiolojia ya Urusi, tayari madhara yameripotiwa katika mikoa iliyoko karibu na kitovu cha tetemeko hilo, ambapo wakazi wamelazimika kuhama makazi yao.
Mawimbi ya tsunami yenye urefu wa hadi mita 30 yameripotiwa kufika kwenye visiwa vya Hokkaido nchini Japan na visiwa vya Kuril vinavyodhibitiwa na Urusi. SOMA: Waliokufa kwa tetemeko la ardhi wafikia 161 Japan
Aidha, mataifa mengine kama Ufilipino, Chile na Visiwa vya Solomon yameongeza tahadhari ya tsunami, huku Marekani ikitazamiwa kupata athari zake hususan kwenye miji ya California na Washington. Maafisa wa usalama na maafa wanaendelea kufuatilia hali hiyo kwa



