Waliokufa kwa tetemeko la ardhi wafikia 161 Japan

IDADI ya watu waliokufa kutokana na tetemeko la ardhi lililosababisha uharibifu mkubwa Siku ya Mwaka Mpya nchini Japan imeongezeka kufikia zaidi ya 160, mamlaka zilisema.

Juhudi zinaendelea kuwatafuta zaidi ya watu 100 ambao walitoweka wiki moja baadaye.

Imeripotiwa kuwa hali mbaya ya hewa inawapa changamoto waokoaji, mvua kubwa na theluji inasababisha maporomoko yanayokwamisha zoezi la uokoaji.

Tetemeko hilo lenye ukubwa wa 7.

6 katika kipimo cha Richter lilipiga Peninsula ya mbali ya Noto na kuangusha majengo na kuzua moto mkubwa.

Idadi kubwa ya vifo vimetokea katika miji iliyoathirika sana ya Wajima na Suzu.

Wakati huo huo, idadi ya watu waliokuwa hawaonekani imepungua kutoka 195 hadi zaidi ya 100.

Idadi ya vifo imeongezeka kutoka 120 iliyoripotiwa Jumapili.

Jeshi la Japan limekuwa likitoa vifaa vikiwemo chakula, maji na blanketi kwa ajili ya wale ambao wamelazimika kuyahama makazi yao.

Habari Zifananazo

Back to top button