Sudan Kusini yapoteza askari 5 mpakani

JUBA : TAKRIBAN askari watano wa Sudan Kusini wameuawa katika mapigano na Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Uganda (UPDF) yaliyozuka mapema wiki hii katika mpaka wa nchi hizo mbili.

Maafisa wa eneo hilo walithibitisha tukio hilo siku ya Jumatano, wakieleza kuwa mapigano hayo yalitokea Jumatatu katika Jimbo la Equatoria ya Kati, ingawa haijabainika wazi chanzo chake.

Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Sudan Kusini (SSPDF) limethibitisha kutokea kwa mapigano hayo baina ya majeshi hayo mawili ya mataifa jirani. SOMA: Mazungumzo ya amani Sudan Kusini yaanza

Uganda imekuwa mshirika muhimu wa usalama nchini Sudan Kusini na kwa muda mrefu imekuwa ikitoa msaada wa kijeshi kwa serikali ya Rais Salva Kiir. Miongoni mwa hatua zilizochukuliwa na Uganda ni pamoja na kutuma vikosi maalum nchini humo tangu mwezi Machi mwaka huu.

 

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button