Mazungumzo ya amani Sudan Kusini yaanza

KENYA : MAZUNGUMZO ya amani ya Sudan Kusini yaliyopewa jina la Tumaini yameanza tena nchini Kenya baada ya kukwama kwa miezi minne iliyopita.

Hizi ni jitihada zinazofanywa hivi karibuni za kumaliza mzozo huo ambao kwa muda mrefu umedumaza uchumi wa nchi hiyo.

Hapo jana, mpatanishi mkuu wa  mazungumzo hayo Lazarus Sumbeiyo alizitaka pande zote mbili kukubaliana kumaliza  vita ya wenyewe kwa wenyewe nchini humo.

Mkuu wa Muungano wa Upinzani wa Sudan Kusini, Pagan Amum amesema anataka kuona mazungumzo hayo yanazingatia yale yanayohitajika ili kuokoa nchi hiyo kutosambaratika.

Kwa upande wake, Kuol Manyang Juuk, kutoka upande wa serikali, azihimiza pande hizo mbili kuweka kando tofauti zao. SOMA: Sudan Kusini waahirisha uchaguzi Desemba 2026

 

 

Habari Zifananazo

Back to top button