SUDAN KUSINI : RAIS wa Sudan Kusini, Salva Kiir ametangaza uchaguzi mkuu utafanyika Desemba 2026 kutokana na kuchelewa kwa maandalizi ya uchaguzi.
Taraifa hii imeifanya, Umoja wa Mataifa kutoa wito kwa viongozi wa Sudan Kusini kuonyesha dhamira yao ya dhati ya kuelekea uchaguzi wa kidemokrasia ili kuleta mageuzi ya kisiasa yatakayoleta tija nchini humo
Balozi wa Umoja wa Mataifa nchini humo Nicholas Haysom, amesema ucheleweshaji huo wa uchaguzi utawasikitisha raia wa nchi hiyo wanaotarajia kuona mageuzi ya siasa nchini humo.
Sudan Kusini ni miongoni mwa taifa changa ambalo linapitia changamoto nyingi za mivutano ya kisiasa kwa muda mrefu hali inayosababisha kudhorotesha ustawi wa maendeleo ya nchi hiyo.