Mwanasheria wa Hakimi acharuka kesi ya ubakaji

PARIS: MWANASHERIA wa Achraf Hakimi, Fanny Colin, anasema kuna “ushahidi mkubwa” ambao unamuondolea tuhuma za ubakaji, huku waendesha mashtaka Ufaransa wakiomba rasmi kesi ya ubakaji dhidi yake ifanyiwe kazi.

“Tutapambana hadi mwisho ili kuhakikisha ukweli unajulikana Achraf Hakimi hakufanya kosa lolote wala kitu chochote kibaya,” Colin aliiambia RMC Sport.

Kesi hiyo ilianza Februari 2023, wakati mwanamke mwenye umri wa miaka 24 alipomshtaki Hakimi kwa kumlazimisha kufanya ngono bila ridhaa nyumbani kwake karibu na Paris.

Ofisi ya mwendesha mashtaka huko Nanterre iliomba Ijumaa Hakimi ahukumiwe na mahakama ya uhalifu.

Hakimi amekanusha vikali madai hayo tangu kuanza kwa uchunguzi.

Sasa, uamuzi uko kwa hakimu anayechunguza kesi hiyo, ambaye ataamua ikiwa kesi hiyo itasikilizwa. Iwapo atapatikana na hatia, Hakimi anaweza kufungwa jela hadi miaka 15.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button